Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji

Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria

WATUMISHI LVBWB WASHIRIKI MAFUNZO

Imewekwa: 12 February, 2026
WATUMISHI LVBWB WASHIRIKI MAFUNZO

Watumishi wa Bodi ya Maji ya Bonde la Ziwa Victoria wameshiriki mafunzo kuhusu Mpango wa Usimamizi Shirikishi na Uendelezaji wa Rasilimali za Maji (IWRMDP), yenye lengo la kuimarisha upangaji, usimamizi na uhifadhi endelevu wa rasilimali za maji katika Bonde la Ziwa Victoria.

Mpango huu umeandaliwa na Bureau for Industrial Cooperation (BICO) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, chini ya Ndaki ya Uhandisi na Teknolojia (CoET). 

Kupitia mafunzo hayo, wataalam wa Bodi walipatiwa uelewa wa kina na kushiriki katika mapitio ya mpango huo, hususan kipengele cha ubora wa maji, kwa lengo la kuhakikisha rasilimali za maji katika Bonde la Ziwa Victoria zinahifadhiwa, zinadhibitiwa kwa ufanisi, na zinatumika kwa usalama na uendelevu.